Wakati Sasa Umeshafika

Wakati Sasa Umeshafika
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumViuzeni Mlivyo Navyo
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerV. B. Kanuti

Wakati Sasa Umeshafika Lyrics

{ Wakati sasa umeshafika wa kujifikiria
Kitu gani umtolee Bwana kama shukrani zako } *2
{ Toa kwa moyo wa mapendo,
Toa ulicho nacho (ndugu) toa kwa ukarimu
Mungu anakuona ndugu mpaka moyoni mwako } *2

 1. Ewe ndugu usimame, nenda mbele zake Bwana
  Kamtolee sadaka Bwana kwa mapendo yote
 2. Tolea moyo wako, pamoja na matendo yako
  Naye Bwana Mungu wako kweli atakubariki
 3. Siku zote Mungu wako amekulinda vyema
  Nawe sasa ndugu yangu hima ujifikirie
 4. Baraka zake Mungu za Baba na za Mwana
  Na za Roho Mtakatifu ziwe nanyi siku zote