Huu Sasa Ni Wakati

Huu Sasa Ni Wakati
Performed bySt. Mary Viane Bulanda Busia
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,657

Huu Sasa Ni Wakati Lyrics

  1. Huu sasa ni wakati wa kufikiri
    Kwa moyo pia hata na matendo yako
    Umtolee Mungu sadaka ya leo

    Mkate divai - pokea, mazao yetu - pokea
    Na fedha zetu -pokea, zikupendeze - pokea (Pokea Baba)
    {Hivi vyote tunavyoleta Baba Mungu pokea
    Ni kazi yetu sisi Bwana Baba uvibariki
    Baba zikupendeze zawadi tunaleta } *2

  2. Jifikirie ndugu utakachotoa,
    Kwa moyo pia hata na matendo yako
    Umtolee Mungu sadaka ya leo
  3. Mtolee Mungu sadaka yako leo
    Atakupa zaidi ya unayotaka
    Umtolee Mungu sadaka ya leo