Waumini Tuwe na Juhudi
| Waumini Tuwe na Juhudi |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Offertory/Sadaka |
| Composer | John Mgandu |
| Views | 4,077 |
Waumini Tuwe na Juhudi Lyrics
Waamini tuwe na juhudi kulijenga kanisa letu *2
{ Tutoe kwa ukarimu, sehemu ya mali yetu
Aliyotujalia Mwenyezi Mungu } *2
- Waumini tuwe tayari daima kujitolea kwa hali na mali
Na kwa ukarimu sote tulijenge kanisa letu
- Waumini amkeni tuwajibike kulijenga hekalu la Mungu
Ndiyo nyumba ya sala na ibada takatifu
- Kanisa litajengwa na sisi wenyewe, kwa hivyo waumini
Tufanye juhudi kutoa michango yetu