Mali Yako
Mali Yako Lyrics
- Mali yako Mali Yako, Mali yako,
na vinatoka kwako vyote mali yako na vinatoka kwako
Mkate wetu nayo divai yetu Dhabihu zetu
nayo divai yetu mali yako mali yako mali yako
- Mali yako nguvu zangu na uhai wangu
familia na jamii yangu Fedha nilizonazo
ni zako mazao nivunayo ni yako
Milele! Mi- Mi- Milele (Utukuzwe utukuzwe Bwana Mungu milele) x 2
Maana kwa wema wako tumepokea huu mkate na kutoka kwako tumepokea hii divai.
- Mali yako:Umri wangu na ujana wangu
Shida zangu furaha zangu
Na vipaji vyangu vyote x2
- Mali yako:Ndoa yangu na uchumba wangu
Utume ukasisi na utawa wangu
Mwili na roho yangu ni vyako x2
- Mali yako:Utajiri na elimu yangu
Umaarufu wangu mkubwa
Hadhi niliyo nayo ni yako,
Unyonge wangu pia ni wako