Wakati Sasa Umefika
Wakati Sasa Umefika Lyrics
Wakati sasa umefika, wa kutoa sadaka
Amka ndugu tupeleke, sadaka zetu kwake
Ni mema mengi sana kila siku anatugawia
Lakini tunshindwa kumshukuru Mungu Baba
Twendeni kwa pamoja tupeleke sadaka zetu
Tutoe kwa upendo Mungu Baba atapokea
- Ee ndugu fikiria maisha yako yote
Tangu kuumbwa kwako na bado unaishi
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
- Usiku na mchana hachoki kutulinda
Tukiwa na safari ajali aepusha
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
- Uwezo wako wote umepewa na Mungu
Na kazi ufanyazo Mungu amebariki
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
- Mapato yako yote yanatoka kwa Bwana
Ingawa ni kidogo Bwana atapokea
Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka