Twaja Kwako Bwana

Twaja Kwako Bwana
Performed bySt. Monica Lower Kabete Campus UoN
AlbumUwe Nami Bwana
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerJohnBosco Hosea
Views4,879

Twaja Kwako Bwana Lyrics

  1. Twaja kwako Bwana (leo) kwa furaha kubwa (sisi)
    Twaleta zawadi Bwana tukushukuru
    Kwa Baraka zako (zote) nayo mema yako (kwetu)
    Kweli u mkarimu Bwana masihani mwetu.

    Twajitoa kwako, Bwana utupokee sisi
    Japo hatustahili, twaja ututakase
    Nafsi zetu sisi, twazitoa kwako ee Bwana
    Ili iwe ishara, ya shukrani zetu kwako

  2. Mkate mazao ya ngano, tunakutolea Bwana
    Upate kugeuza uwe mwili wako Bwana.
    Kutoka kwa mizabibu tunaleta na divai, Bwana uigeuze
    Iwe kinywaji cha roho, tupate uzima wako
  3. Kutoka kwa mifuko yetu, tunakutolea fedha
    Kama fungu la kumi, Bwana zibariki zote
    Kutokana na bidii zetu tunakutolea mazao ya mashamba
    Kutoka kwa boma zetu, twaleta mifugo kwako
  4. Tunajitoa kwako Bwana kwa nafsi na maisha yetu,
    Pia na nguvu zetu tuwe watumishi wako
    Mioyo yetu twaleta kwako tupokee Bwana, sisi ni waja wako
    Tutumie jinsi wewe utakavyopenda Bwana.
  5. Zawadi tuletazo kwako kwa moyo wa ukarimu
    Tunakuomba Bwana nazo zipokee kwako
    Utujalie Baraka pia na fadhili zako, wewe ni Mungu wetu
    Nasi tutaishi daima ndani yako Baba yetu