Login | Register

Sauti za Kuimba

Twaja Kwako Bwana Lyrics

TWAJA KWAKO BWANA

@ JohnBosco Hosea

Twaja kwako Bwana (leo) kwa furaha kubwa (sisi)
Twaleta zawadi Bwana tukushukuru
Kwa Baraka zako (zote) nayo mema yako (kwetu)
Kweli u mkarimu Bwana masihani mwetu.

Twajitoa kwako, Bwana utupokee sisi
Japo hatustahili, twaja ututakase
Nafsi zetu sisi, twazitoa kwako ee Bwana
Ili iwe ishara, ya shukrani zetu kwako

 1. Mkate mazao ya ngano, tunakutolea Bwana
  Upate kugeuza uwe mwili wako Bwana.
  Kutoka kwa mizabibu tunaleta na divai, Bwana uigeuze
  Iwe kinywaji cha roho, tupate uzima wako
 2. Kutoka kwa mifuko yetu, tunakutolea fedha
  Kama fungu la kumi, Bwana zibariki zote
  Kutokana na bidii zetu tunakutolea mazao ya mashamba
  Kutoka kwa boma zetu, twaleta mifugo kwako
 3. Tunajitoa kwako Bwana kwa nafsi na maisha yetu,
  Pia na nguvu zetu tuwe watumishi wako
  Mioyo yetu twaleta kwako tupokee Bwana, sisi ni waja wako
  Tutumie jinsi wewe utakavyopenda Bwana.
 4. Zawadi tuletazo kwako kwa moyo wa ukarimu
  Tunakuomba Bwana nazo zipokee kwako
  Utujalie Baraka pia na fadhili zako, wewe ni Mungu wetu
  Nasi tutaishi daima ndani yako Baba yetu
Twaja Kwako Bwana
COMPOSERJohnBosco Hosea
CHOIRSt. Monica Lower Kabete Campus UoN
ALBUMUwe Nami Bwana
CATEGORYOffertory/Sadaka
 • Comments