Mpeni Kaisari
Mpeni Kaisari Lyrics
- Vipaji tumepewa, mapato tumepata
Lakini binadamu tunashindwa kushukuru
Wakati tunaomba, tunajinyenyekesha
Lakini tukipata mikono yetu birika
Mpeni kaisari, yaliyo yake
Mpeni Mungu (yale) yaliyo yake Mungu *2
- Mifugo tunafuga, nafaka tunavuna
Lakini kila siku tunakula na kusaza
Kumbuka kuna wale, wasio na chochote
Hawawezi kupata, hata kikombe cha chai
- Tunapofanya kazi, twapata mishahara
Shughuli zetu sisi kuingia kwenye baa
Ikiwa zitabaki, twakuja kanisani
Twamtolea Mungu, shilingi moja na tano
- Tukiwa na wagonjwa hatuwasaidii
Wakati wamekufa tunachanga kwa huzuni
Twachukua mikopo, kwa mambo ya anasa
Ujenzi wa kanisa, twalazimishwa kutoa.
- Kumbuka Ibrahimu, alitoa mwanawe
Kama sadaka kwake Mungu Baba wa mbinguni
Na sisi kwa furaha, tupeleke zawadi
Itakayopendeza, kama ile ya Abeli