Acheni Visingizio
Acheni Visingizio |
---|
Performed by | - |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | Deo Kidaha |
Views | 19,075 |
Acheni Visingizio Lyrics
Acheni visingizio wanadamu,
acheni visingizio kwamba hali ni ngumu * 2
Nendeni mkatoe (vipaji) nendeni mkatoe vipaji
nendeni mkatoe vipaji kwa Bwana * 2
- Siyo ninyi wenye magari ya kifahari mnaodai hali ni ngumu.
Siyo ninyi wenye fedha nyingi mifukoni mnaodai hali ni ngumu.
- Siyo ninyi wenye majumba ya kifahari mnaodai hali ni ngumu.
Ndani yake mmejaza vito vya thamani mnaodai hali ni ngumu.
- Siyo ninyi mnaovuna mazao mengi mnaodai hali ni ngumu.
Siyo ninyi mnaopokea mishahara mnaodai hali ni ngumu.
- Msidhani mmepata kwa uwezo wenu mnaodai hali ni ngumu.
Bali ni Mungu aliye wajalia hayo mnaodai hali ni ngumu.
- Kumbukeni mjane alotoa dinari mnaodai hali ni ngumu.
Hakubakiza chochote mfukoni mwake mnaodai hali ni ngumu.