Huu Sasa ni Wakati

Huu Sasa ni Wakati
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumViuzeni Mlivyo Navyo
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerV. B. Kanuti
SourceDar-es-Salaam Tanzania

Huu Sasa ni Wakati Lyrics

Huu sasa ni wakati wa kutoa yako sadaka
Usisite Mungu wako akuona usifiche
Huu sasa ni wakati wa kutoa yako sadaka
Usisite Mungu wako akuona usifiche

{Toa ndugu toa, toa ndugu toa ndugu
Ulicho nacho, mshukuru Mungu wako kwa mema yote} *2

  1. Mtolee shukrani zako Mungu wako
    Kwa kutoa zawadi uliyo nayo
  2. Ulivyo navyo amekupa Yeye Bwana
    Nawe mpe Bwana kwa shukrani
  3. Nafsi zetu na mali pia vyake Bwana
    Haki kuvirudisha kwake Bwana