Sadaka ya Kuazima
| Sadaka ya Kuazima |
|---|
| Alt Title | Jiandae Kutoa Sadaka |
| Performed by | - |
| Category | Offertory/Sadaka |
| Composer | Martin M. Munywoki |
| Views | 3,831 |
Sadaka ya Kuazima Lyrics
Jiandae wiki nzima weka tayari
sadaka yako mkristu (toa kwa moyo safi)
Usitoe kwa uchoyo wala sadaka ya kuazima
{(jasho lako) umtolee Mungu alicho kupa hahitaji zaidi
(maana) Vitu vyote mali yake toa kwa ukarimu } *2
- Ninaona hasara kutoa (nanung'unika)
Bwana ona mi nilivyo changanyikiwa
Mara nyingi naomba jirani (hapa kitini)
siyo yangu ni sadaka ya kuazima
- Ninaona uchoyo kutoa (sadaka yangu)
ninaleta kidogo tena kwa uchungu
Mara nyingine sitoi kitu (nilicho nacho)
ninaficha sadaka yangu mfukoni
- Ninaona aibu kubaki (ni wasiwasi)
nimeketi nao wengine wanatoa
Mara nyingine hata siendi (nimekimbia)
kanisani ninahepa michango nyingi
- Wana baraka wanaotoa (kwa moyo ule )
wa Abeli wa Ibrahimu na Isaka
Bwana Mungu haipendi sadaka (yake Kaini)
wala yule Anania na Safira