Leteni Sadaka Kamili
Leteni Sadaka Kamili | |
---|---|
Performed by | St. Monica Lower Kabete Campus UoN |
Album | Toba Yangu |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | Pius Kalimsenga |
Views | 19,534 |
Leteni Sadaka Kamili Lyrics
Leteni sadaka kamili ghalani *2
{ Ili chakula kiwemo katika nyumba yangu,
Asema Bwana, Bwana wa majeshi } *2- Mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana
Nitafungua milango ya mbingu, asema Bwana
Na kuwamwagia baraka tele, asema Bwana - Mimi ndimi mgawa wa vipaji, asema bwana
Nitawaongezea maarifa, asema Bwana
Ya kuyashinda magumu yoyote, asema Bwana - Mtakachokiomba nitawapa, asema bwana
Nitawapa vyeo na mali nyingi, asema Bwana
Nakuuondoa umasikini, asema Bwana - Nitawalinda na kuwasitawisha, asema Bwana
Nanyi mtazaa matunda bora, asema Bwana
Yatakayo dumu milele yote, asema Bwana