Angalieni Msifanye Wema
| Angalieni Msifanye Wema | |
|---|---|
| Performed by | St. Francis of Assisi Msimbazi | 
| Category | Offertory/Sadaka | 
| Composer | Stanslaus Mujwahuki | 
| Views | 4,184 | 
Angalieni Msifanye Wema Lyrics
- Angalieni msifanye wema wenu,
 Msifanye wema wenu machoni mwa watu,
 Ili mtazamwe nao,
 Kwa maana, mkifanya hivyo hampati
 dhawabu kwa baba yenu aliye Mbinguni
- Basi wewe utoapo sadaka,
 Usipige panda mbele yako,
 Kama wanafiki wafanyavyo,
 katika masinagogi na njiani,
 Ili watukuzwe na watu.
- Amin amin nawaambieni,
 Wamekwisha pata dhawabu yao,
 Bali wewe utoapo sadaka,
 Hata mkono wako wa kushoto usijue,
 Ufanyalo mkono wako wa kuume.
 
  
         
                            