Sadaka Yetu Bwana
| Sadaka Yetu Bwana |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Offertory/Sadaka |
| Composer | Dan Odhiambo |
| Views | 5,873 |
Sadaka Yetu Bwana Lyrics
Sadaka yetu Bwana, twaomba upokee
Ni mazao ya mashamba yetu ee Baba upokee *2
- Mkate na divai, na pia nafsi zetu
Ni zawadi yetu kwako, ee Baba upokee
- Na fedha za mifukoni,mazao ya mashamba,
Ee Baba, kazi zetu, twaomba upokee(sadaka)
- Pokea na nyoyo zetu, miili yetu pia
Ee Baba utupokee, tulio wana wako(sadaka)
- Pokea tunakuomba, ingawa ni kidogo
Kwa unyenyekevu Baba, tunavileta kwako
- Zawadi hii twaitoa, kwa sifa yako wewe,
Kwa ajili yetu sisi, nazo jamaa wetu (sadaka)