Sala Yangu Ipae
Sala Yangu Ipae | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | L. Komba |
Views | 39,246 |
Sala Yangu Ipae Lyrics
Sala yangu ipae mbele yako Bwana * 2
{ Kama moshi wa ubani altareni,
Na kuinuliwa kwa mikono yangu
Iwe kama sadaka, sadaka ya jioni } * 2- Ee Bwana tunakutolea sadaka yetu,
Pamoja na maisha ya kila siku. - Uwe radhi kuipokea sadaka yetu,
Kama zile za mababu wa zamani. - Hivyo sadaka ifane mbele zako Bwana,
Na iwe sadaka ya shukrani kubwa. - Nasi utubariki maisha yetu yote,
Na mwisho utujalie heri yako.