Hazina ya Mbinguni
Hazina ya Mbinguni |
---|
Performed by | - |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | D. Wasonga |
Views | 4,452 |
Hazina ya Mbinguni Lyrics
- Hiki ndicho nilichoandaa, siku ya leo
(Nami) nakusihi ukipokee
Hii ndiyo shukrani yangu, sehemu ya pato langu
Itokayo ndani ya mtima wangu
Hivyo, naileta mikononi mwako (ambapo) nondo hawataiharibu (na kutu)
Naileta mikononi mwako, ambapo mwizi hawezi kuiba
naileta mahali salama iwe hazina yangu mbinguni
- Ninakutolea moyo wangu wala si mifuko yangu
Ndiyo kazi ya mikono yangu, nakusihi uibariki
- Hata kama ni kidogo nakusihi ukipokee
Kwani ndicho nilichoandaa kukutolea ee Mungu wangu
- Hiki ninachokutolea kikekupendeze Mungu wangu
Kama ile sadaka ya mtumishi wako, mtumishi wako Abeli