Leteni Ndama Wanono
Leteni Ndama Wanono |
---|
Performed by | - |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | F. Mtegeta |
Views | 22,036 |
Leteni Ndama Wanono Lyrics
- Leteni ndama walionona madhabahuni kwa Bwana tena
Toeni bila kinyongo moyoni ndipo mtabarikiwa naye * 2
- Leteni ndama aliyeshiba majani ya kondeni,
mkamtolee Mungu Baba yenu kwa shukrani.
- Peleka sadaka yako iliyo safi na ya kupendeza,
ndipo utakapokitikisa kiti cha mwenyezi.
- Kumbuka yule mjane aliyetoa senti moja,
alibarikiwa na kuongezewa na mwenyezi.
- Sadaka iliyo safi ni ile inayokugusa wewe,
hiyo ndiyo sadaka iliyo safi sana.
- Isaka alitolewa na baba yake kama sadaka,
hivyo Abrahamu alizidishiwa uzao wake.