Leteni Ndama Wanono

Leteni Ndama Wanono
ChoirTBA
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerF. Mtegeta

Leteni Ndama Wanono Lyrics

Leteni ndama walionona madhabahuni kwa Bwana tena
Toeni bila kinyongo moyoni ndipo mtabarikiwa naye * 2

 1. Leteni ndama aliyeshiba majani ya kondeni,
  mkamtolee Mungu Baba yenu kwa shukrani.
 2. Peleka sadaka yako iliyo safi na ya kupendeza,
  ndipo utakapokitikisa kiti cha mwenyezi.
 3. Kumbuka yule mjane aliyetoa senti moja,
  alibarikiwa na kuongezewa na mwenyezi.
 4. Sadaka iliyo safi ni ile inayokugusa wewe,
  hiyo ndiyo sadaka iliyo safi sana.
 5. Isaka alitolewa na baba yake kama sadaka,
  hivyo Abrahamu alizidishiwa uzao wake.

Favorite Catholic Skiza Tunes