Vipaji Hivi
   
    
     
         
          
            Vipaji Hivi Lyrics
 
             
            
- { Vipaji hivi ni kama dhabihu yenye harufu nzuri (nzuri)
 Sadaka inayokubaliwa na kumpendeza Mungu } *2
 {(tutoe) Kwa furaha tutoe (tutoe)
 (tutoe) Kwa imani tutoe (tutoe)
 (tutoe) Kwa mapendo tutoe (tutoe)
 Na tutoe kwa shukrani } *2
- Tupeleke, mazao ya shamba
 Tupeleke. nayo mifugo
 Tupeleke, vilivyo vinono
 Kama sadaka ya Abeli
- Nazo fedha, ni mali ya Bwana
 Tumepata, kwa neema zake
 Tupeleke, kwa moyo wa sala
 Tupeleke, shukrani zetu
- Tupeleke, nazo nafsi zetu
 Tupeleke, kama dhabihu
 Tumwombe Mungu atubariki
 Tukatende, impendezavyo