Vipaji Hivi

Vipaji Hivi
ChoirSauti Tamu Melodies
AlbumNyimbo za Matoleo
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerCharles Saasita
VideoWatch on YouTube

Vipaji Hivi Lyrics

 1. { Vipaji hivi ni kama dhabihu yenye harufu nzuri (nzuri)
  Sadaka inayokubaliwa na kumpendeza Mungu } *2
  {(tutoe) Kwa furaha tutoe (tutoe)
  (tutoe) Kwa imani tutoe (tutoe)
  (tutoe) Kwa mapendo tutoe (tutoe)
  Na tutoe kwa shukrani } *2

 2. Tupeleke, mazao ya shamba
  Tupeleke. nayo mifugo
  Tupeleke, vilivyo vinono
  Kama sadaka ya Abeli
 3. Nazo fedha, ni mali ya Bwana
  Tumepata, kwa neema zake
  Tupeleke, kwa moyo wa sala
  Tupeleke, shukrani zetu
 4. Tupeleke, nazo nafsi zetu
  Tupeleke, kama dhabihu
  Tumwombe Mungu atubariki
  Tukatende, impendezavyo